Msanii wa Endless Fame Films, Mirror amesema alimrekodi Nuh Mziwanda wakati akimtongoza bosi wake Wema Sepetu sababu hakupendezwa na kitendo hicho alichokiona kama ni utovu wa nidhamu.
Akizungumza kwenye kipindi cha Friday Night Live cha EATV, Mirror alisema hawezi kufurahi kumuona ‘dogo’ tu akimtongoza bosi wake.
“Mimi sina matatizo na Nuh cha kwanza na sikurekodi kwa nia ya watu wasikilize,” alisema. “Kwa sababu hata tukiongea ukweli Nuh na madam ni vitu viwili tofauti, [Wema] ni boss, mkubwa hata kwangu. Mimi nilikuwa naangalia movies na sikurekodi kwa nia hata kama akija kusikia girlfriend wake ajue Nuh ndio alikuwa anamsumbua madam,” aliongeza.
“Sijawahi kusikia mtu mwingine akimtongoza madam, siwezi kufurahi Nuh akimtongoza bosi wangu kwa sababu yeye ni dogo kama mimi, halafu yeye ana mwanamke wake
BOFYA HAPA KUMSIKILIZA NUH MZIWANDA AKIMTONGOZA WEMA
Post a Comment